
ZIARA YA MHE DKT SAADA MKUYA SHIRIKA LA BIMA LA ZANZIBAR
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Mheshimiwa Dkt. Saada Mkuya Salum ametembelea Taasisi ya Shirika la Bima la Zanzibar. Waziri Dkt. Saada ameliagiza shirika la Bima kuharakisha kuzindua Bima ya Kiislamu [TAKAFUL] ili ianze kazi rasmi hapa Zanzibar.
Mheshimiwa Dkt. Saada ameliagiza shirika la Bima kuhakikisha wanaangalia maeneo ambayo ni kipao mbele cha Serikali ikiwemo eneo la Uchumi wa buluu kwani kwa sasa kuna upungufu mkubwa wa kuvisajili vyombo vya baharini vya kuvulia. Amesema usajili huo wa vyombo hivyo vya baharini uambatane kwa kukatiwa bima ili Serikali ipate mapato yake na kupelekea kukua kwa Uchumi lakini pia kuwawekea usalama Wananchi wetu.
Nae Mkurugenzi Mtendaji ameelezea majukumu yake na baadhi ya changamoto ambazo zinaikabili shirika hilo ikiwemo baadhi ya Wizara za Serikali hawalipi madeni wanayodaiwa na kupelekea kulirudisha nyuma shirika hilo. Mkurugenzi Mtendaji ameyachukuwa yale yote aliyoelekezwa na Mheshimiwa ili kuleta ufanisi wa shirika hilo.